LUANDA VILLA IKO KWA NAFASI NZURI MSIMU HUU

Kocha wa Luanda Villa Gilbert Selebwa ana imani kwamba kikosi chake kimejitayarisha vilivyo kukabiliana na 3KFC ya Embu na kuibuka washindi katika mechi yao ya pili ya ligi Ya kitaifa DARAJA LA PILI NSL iliyoratibiwa Jumapili hii.
Selebwa anasema ushindi dhidi ya timu bora zaidi Kibera Blackstars ni dhihirisho kwamba anaweza kuandikisha ushindi wake wa pili ugenini dhidi ya 3KFC ambao waliilaza Kisumu Allstars 4-0 wikendi iliyopita.
Hata hivyo, Selebwa anatakiwa kubadili mbinu ili kuwavutia mashabiki wa Luanda Villa FC waliomwona akihangaika kupata ushindi kwenye uwanja wa Mumboha Sports wikendi iliyopita.
Bado haijabainika iwapo nahodha wa Luanda Villa Clinton Odiwuor ambaye alipata jeraha wakati wa mchuano wa Kibera Blackstars ugani Mumboha atashiriki dhidi ya 3KFC.
Luanda Villa ambao wanashiriki Ligi ya Taifa ya Super League kwa mara ya pili watakuwa wakimenyana na washiriki wa mara ya kwanza 3KFC ambao walizua hofu wikendi iliyopita kwa kuwazaba Kisumu Allstars 4-0 ugenini.
Imetayarishwa na Nelson Andati