NI UONGO, WANAHARAKATI WAMJIBU KINDIKI

Vuta nikuvute inaendelea baina ya serikali na wanaharakati kuhusiana na lengo la maandamano ya kizazi cha Gen Z yaliyoshuhudiwa nchini katika mwezi wa Juni na Julai mwaka huu, wanaharakati sasa wakipinga madai ya waziri wa usalama Kithure Kindiki kwamba walikuwa na lengo la kupindua serikali kupitia mandamano hayo.
Katika mahojiano na kituo kimoja cha runinga mapema leo, Kasmuel Mcoure aliyekuwa msitari wa mbele kwenye maandamano hayo, amesema maandamano hayo yalilenga kupinga uongozi mbaya serikalini.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa