WAZIRI BARASA:UTAPOKEA HUDUMA ZA BURE, IKIWA UMESAJILIWA CHINI YA SHA

Wakenya ambao watajisajili katika bima mpya ya afya watapata huduma za matibabu katika hosipitali za umma.
Waziri wa Afya Dkt. Deborah Barasa amewataka Wakenya kujitokeza kwa wingi na kujisajili kwenye mpango uliozinduliwa wa bima ya Afya ya Jamii (SHIF), akisema itawahudumia Wakenya wote kwa kiwango cha chini.
Akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa mpango wa Mamlaka ya Afya ya Kijamii (SHA) mjini Eldoret, Barasa amesema pindi tu kusajiliwa, Wakenya watapokea dawa bila malipo kutoka kwa vituo vya chini vya afya vya umma.
Imetayarishwa na Janice Marete