CHUO KIKUU CHA MOI CHAFUNGWA

Shughuli za masomo zimefutiliwa mbali katika chuo kikuu cha Moi kutokana na mgomo wa wahadhiri ambao hatimaye umesababisha maandamano ya wanafunzi.
Kupitia waraka, mkuu wa chuo hicho Isaac Kosgey ameagiza kufungwa mara moja kwa chuo hicho, akifutilia mbali shughuli za masomo kwa muhula wa kwanza wa kati ya Septemba na Disemba.
Aidha, amewataka wanafunzi wote kuondoka chuoni humo mara moja.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa