MAHAKAMA YASITISHA UTEKELEZWAJI WA MFUMO MPYA WA UFADHILI WA ELIMU YA JUU

Utawala wa Rais William Ruto umepata pigo kubwa katika azma yake ya kutoa elimu bora baada ya Mahakama Kuu kusitisha utekelezaji wa mtindo mpya wa ufadhili wa vyuo vikuu.
Katika uamuzi wake, Jaji Chacha Mwita ameamuru mfumo huo kusimamishwa kwa muda kusubiri kusikilizwa na kuamuliwa kwa kesi iliyowasilishwa na Tume ya Haki za Kibinadamu ya Kenya (KHRC)
Jaji huyo amebainisha kuwa kesi hiyo ilicheleweshwa kwa muda mrefu kutokana na Mwanasheria Mkuu.
Waziri wa Elimu na Huduma ya Upangaji wa Vyuo Vikuu vya Kenya (KUCCPS) kuchelewa kuwasilisha mawasilisho yao.
Imetayarishwa na Janice Marete