SERIKALI YA TURKANA YAENDESHA CHANJO YA POLIO

Katika juhudi za kukabili kuenea kwa ugonjwa wa Polio ambao umerekodiwa katika kaunti ya Turkana, serikali ya kaunti hiyo imeanzisha chanjo dhidi ya ugonjwa huo huku wakazi wakihimizwa kuwawasilisha wanao kwa zoezi hilo.
Kwa mujibu wa wizara ya afya, kati ya visa 5 vilivyoripotiwa nchini, 4 vimegunduliwa kwenye kaunti hiyo, Watoto walio chini ya miaka 10 wakilengwa kwenye utoaji wa chanjo hiyo.
Zoezi hilo linaongozwa na Waziri wa afya kwenye kaunti hiyo James Long’ole.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa