SHIRIKA LA RELI LA KENYA KRC LABORESHA MIUNDO MBINU YA SGR
Abiria wanaotumia usafiri wa reli ya kisasa SGR humu nchini watasafiri kwa urahisi baada miundo mbinu ya reli hiyo kuimarishwa kote nchini.
Kuimarishwa Shirika la Reli la Kenya (KRC) limetoa taarifa likisema huduma ya reli ya SGR iliyojengwa na China nchini Kenya, imeboreshwa baada ya kuongezwa kwa mabehewa mapya ya daraja la juu. Hatua hiyo inatarajiwa kuboresha huduma kwa abiria katika sekta mbalimbali ikiwemo ufanisi, anasa, usalama na urahisi.
KRC imesema kuwa nauli za mabehewa mapya zitabadilika kutegemea umri wa abiria.
Waziri wa Barabara na Uchukuzi Davis Chirchir amehudhuria sherehe ya uzinduzi wa huduma hiyo iliyoboreshwa.
Imetayarishwa na Maureen Amwayi
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































