NCD YAITAKA WIZARA YA AFYA KUHAKIKISHA WAGONJWA WA MAGONJWA SUGU KUSIMAMIWA KIKAMILIFU NA SHA

Wagonjwa wanaougua magonjwa sugu huenda wapatata afueni kwa kusimamiwa gharama ya matibabu iwapo shinikizo la shirika la kuangazia magonjwa yasiyoambukiza nchini NCD kuangazia upya bima mpya ya SHA ili kuhakikisha watu wanaugua magonjwa hayo wanafathiliwa kikamilifu na kupata matibabu.
Kulingana na afisa wa NCD Gedion Ayoda SHA inagharamia huduma ya kuoshwa kwa figo Dialysis mara mbili kwa wiki hali ambayo itawalazimu walio na matatizo ya figo kutafuta mbinu nyingine iwapo watahitaji huduma hiyo mara tatu kwa wiki.
Imetayarishwa na Janice Marete