MITIHANI YA KITAIFA IKO TAYARI ASEMA WAZIRI JULIUS OGAMBA

Watahiniwa wa mitihani ya kitaifa wamehakikishiwa usalama wao wakati wa kufanya mitihani yao
Waziri wa Elimu, Julius Ogamba amehakikisha kuwa mtihani wa kitaifa wa mwaka huu uko salama akiongeza kuwa serikali imeweka mikakati ya kutosha ili kuepuka makosa ya mitihani.
Ogamba, akizungumza katika Kituo cha Mafunzo ya Ufundi cha Siala huko Rongo amesema wizara ya elimu ina nia ya kufanya mtihani bila visa vua udanganyifu kushuhudiwa.
Ogamba ameongeza kuwa yeyote katika sekta ya elimu ambaye atahusika katika udanganyifu wa mitihani atakabiliwa na madhara makubwa ambayo ni pamoja na kufukuzwa.
Waziri ametoa wito kwa watu wote katika sekta ya elimu kuunga mkono serikali katika kufanikisha mtihani wa kitaifa wa kuaminika.
Imetayarishwa na Janice Marete