UTOAJI WA SHA MJINI MOMBASA NI WA KUVUTIA – CS BARASA

Wakenya wamehakikishiwa kuwa watapokea huduma za afya chini ya bima ya afya ya jamii bila tatizo lolote.
Waziri wa afya Deborah Barasa akizungumza katika kaunti ya Mombasa wakati wa tathmini ya vituo vya afya kuhusu utekelezaji wa Mamlaka ya Afya ya Kijamii. amesema kuwa Wagonjwa wanaotafuta huduma ya kusafisha damu katika Hospitali Kuu ya Walimu na Rufaa ya Pwani wanapata huduma bila usumbufu,
Barasa alisema ushirikiano wa serikali ya kitaifa na kaunti, SHA na washikadau wengine umehakikisha wagonjwa wanapata huduma za haraka.
Amesema, hata hivyo, katika kitengo cha saratani, usajili uko nyuma ila hakuna mgonjwa atakayekataliwa.
Imetayarishwa na Janice Marete