JAJI MKUU MARTHA KOOME ATEUA JOPO LA MAJAJI 3 KWA AJILI YA MAOMBI YA KUPINGA KUONDOLEWA KWA NAIBU RAIS GACHAGUA

Ombi la naibu wa rais Rigathi Gachagua kupitia mawakili wake la kutaka jaji mkuu Martha Koome kubuni jopo la majaji kusikiliza kesi ya kubanduliwa mamlakani dhidi yake limejibiwa baada ya jaji mkuu Martha Koome kubuni jopo la majaji watatu watakaosikiliza na kuamua kesi dhidi ya Gachagua.
Jopo hilo litaongozwa na Jaji Erick Ogola, huku majaji Antony Mrima na Dkt Frida Mugambi wakiungana naye.
Naibu Rais Gachagua, akiwakilishwa na timu ya wanasheria inayoongozwa na Wakili Mkuu Paul Muite, anapinga kuondolewa kwa mashtaka kwa misingi kadhaa, ikiwa ni pamoja na ukosefu wa ushiriki wa umma.
Imetayarishwa na Janice Marete