WAZIRI TUYA KUONGOZA SHEREHE ZA 13 ZA KDF

Waziri wa Ulinzi Soipan Tuya leo hiii anatarajiwa ku ongoza vikosi vya kijeshi katika kuadhimisha Maadhimisho ya 13 ya Siku ya Majeshi ya Ulinzi ya Kenya.
Hafla ya 2024 itaadhimishwa eneo la Thika garrison huko Thika, Kaunti ya Kiambu.
Litakuwa tukio muhimu kwa sababu wanajeshi wanajiandaa kurejea nyumbani baada ya kukamilika kwa Misheni yao ya Mpito ya Afrika nchini Somalia (ATMIS) mwezi Desemba.
Itakuwa ni mara ya kwanza kwa Tuya kuwa anaongoza hafla hiyo tangu achukue hatamu za uongozi kama waziri wa ulinzi. Siku ya KDF huadhimishwa kila mwaka ili Kuadhimisha na kusherehekea vitendo vya ushujaa vya mashujaa na wa KDF.
Siku hii maalum imeadhimishwa tangu Oktoba 2012 kufuatia uzinduzi wa Operesheni Linda Nchi Oktoba 2011.
Operesheni hiyo ilibadilisha sura ya KDF, na kuonyesha umahiri wake katika kulinda nchi.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Nguvu Moja, Misheni Tayari: Umoja katika Vitendo kwa Usalama wa Taifa na Maendeleo”
Imetayarishwa na Janice Marete