#Local News

GACHAGUA: CHECHE ZACHACHA SENETI

Vikao vya kusikiliza hoja ya kumbandua kutoka afisini naibu Rais Rigathi Gachagua vimekuwa na mihemko ya hapa na pale, baadhi ya maseneta wakihisi kutengwa katika mchakato wa kuchangia kwenye hoja hiyo.

Mmoja wa maseneta hao ni Seki Lenku wa Kajiado, ambaye amelazimika kuomba msamaha kwa spika wa seneti Amason Kingi baada ya kuibua madai kwamba Kingi anaegemea upande mmoja katika kutoa nafasi kwa wanaochangia.

Wakati uo huo, Kingi amewaonya baadhi ya maseneta kuwa atawatimua kutoka majengo ya seneti kutokana na anachokitaja kuwa ukiukaji wa kanuni zinazoongoza shughuli za seneti.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *