WALIMU 20,000 KUAJIRIWA MWAKANI, RUTO AAHIDI
Shughuli za masomo zinatarajiwa kuimarika zaidi kuanzia Januari mwaka ujao baada ya Rais William Ruto kufichua kwamba serikali ina mpango wa kuwaajiri walimu 20,000 zaidi kuhakikisha kuwa wanafunzi nchini wanapokea elimu bora.
Akizungumza katika Ikulu ya Nairobi, Rais amewataka wazazi kuwekeza pakubwa katika elimu ya wanao, huku serikali ikijizatiti kuwaajiri walimu zaidi.
Aidha, amewahakikishia watahiniwa wa KCSE na KPSEA usalama wao wanapojiandaa kwa mitihani yao.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































