GACHAGUA APATA AFUENI MAHAKAMANI

Aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua amepata afueni ya muda baada ya mahakama kuu kufutilia mbali uamuzi wa seneti kukubaliana na bunge la kitaifa katika kumbandua kutoka afisini jana usiku.
Kwenye uamuzi wake, jaji Chacha Mwita amesema kwamba kesi ya Gachagua inaibua masuala inayohusiana na sheria na yanayohusu umma, na kutoa amri ya kuzuia kutimuliwa kwake pamoja na uteuzi wa mrithi wake hadi tarehe 24 Oktoba.
Aidha, amemwagiza jaji mkuu kubuni jopo litakalosikiliza kesi hiyo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa