KARUA AMTAKA RUTO ‘KUTOWATUMIA’ WANASIASA

Kinara wa Narc Kenya Martha Karua amemtaka Rais William kulinda haki ya kila mkenya wakiwemo viongozi wa kisiasa, mbali na kuheshimu uhuru wa idara ya mahakama.
Akirejelea masaibu ya naibu rais Rigathi Gachagua, Karua amedai kuwa Rais Ruto anawatumia baadhi ya viongozi na kisha kuwatimua kutoka mamlakani.
Aidha, Karua amewataka wabunge kutekeleza majukumu yao ya kikatiba na kujiepusha kutumiwa kisiasa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa