KAUNTI ZAZIDIWA NA MAHANGAIKO

Serikali za kaunti zimeendelea kuibua hofu ya kulemazwa kwa utoaji huduma kutokana na ukosefu wa fedha za kutosha, zikisema kuwa hadi sasa serikali haijawapa mgao wao wa miezi 4.
Kwa mujibu wa gavana wa Makueni Mutula Kilonzo Jr, kucheleweshwa kwa mgao huo kumelemaza utendakazi kwenye kaunti hiyo.
Aidha, amesema hatua hiyo imeongeza gharama ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa