DNA YAASHIRIA MWAKILISHI WADI WAJIR HAJULIKANI ALIKO

Imebainika kwamba mwili uliopatikana katika ziwa Yahud si wa mwakilishi wadi katika bunge la kaunti ya Wajir, Yusuf Hussein Ahmed aliyetoweka mapema mwezi jana.
Hii ni baada ya uchunguzi huru wa sampuli za DNA, ambazo zimeonyesha kuwa mwili huo uliogunduliwa katika mazingira ya kutatanisha ukiwa na majeraha mabaya, ni wa mtu tofauti ambaye hajatambuliwa.
Kwa sasa vikosi vya usalama vinaendelea kushinikizwa kusaidia familia katika kumsaka mwakilishi wadi huyo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa