GACHAGUA: VIKAO VYAREJELEWA KORTINI

Mahakama ya Milimani imerejelea vikao vya kusikiliza kesi kuhusiana na uongozi katika afisi ya naibu rais humu nchini, ikitarajiwa kutoa uamuzi kuhusu ombi la kuondoa maagizo yanayomzuia naibu rais mteule Kithure Kindiki kuingia afisini.
Haya yanajiri wakati ambapo mawakili wa naibu rais aliyetimuliwa Rigathi Gachagua wanaendelea kushinikiza kuvunjwa kwa jopo la majaji 3 linalosikiliza kesi hiyo.
Kulingana na mawakili hao, majaji hao ambao ni Anthony Mrima, Freda Mugambi na Eric Ogolla wanaegemea upande mmoja.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa