BODI YA PPB YAFANYA MSAKO, KUIMARISHA AFYA YA UMMA

Kama njia mojawapo ya kuimarisha afya ya umma na kuwalinda wananchi dhidi ya kudhulumiwa na wahudumu wa afya, bodi ya kudhibiti dawa na sumu nchini imeimarisha juhudi za ukaguzi wa hospitali na vituo vya kuuza dawa kote nchini kuhakikisha sheria zinazingatiwa.
Ukaguzi huo uliaonzia kwa vituo vya kuuza dawa na kisha katika hospitali za level 4, unalenga kuhakikisha sheria zinazodhibiti sekta ya afya zinafuatwa kikamilifu, ikiwemo usambazaji, hifadhi na upeanaji wa dawa.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari, afisa mkuu wa bodi hiyo Julius Kaluai amesema msako huo unafuatia uwepo wa watu wasio na tajriba ya kutosha katika utoaji wa huduma za kimartibabu nchini.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa