ICHUNGWA: MAHAKAMA INAINGILIWA NA WANAHARAKATI WA KUTETEA HAKI ZA BINADAMU

Kiongozi wa wengi katika bunge la kitaifa ameikosoa idara ya mahakama kwa madfai kwamba idara hiyo imekubali kuingiliwa na wanaharakati.
Akizungumza mjini Naivasha katika kongamano la wabunge linaloendelea kwa siku ya pili hii leo ichungwa ambaye pia ni mbunge wa Kikuyu amedai kuwa mahakama zinatumiwa vibaya sheria ya mahitaji ya kushirikisha wananchikwenye maswala ya uongozi ili kuweka vizingiti katika miswada muhimu akitoa mfano wa kuharamishwa kwa mswada wa fedha 2023-2024.
Kauli ya kimani imeungwa mkono na kiongozi wa walio wachache katika bunge la kitaifa Junet Mohamed.
Imetayarishwa na Janice Marete