MAAFISA WA POLISI WAANZISHA MSAKO KUMTAFUTA MWANAMUME ALIYEMUUA BABA YAKE HUKO MIGORI

Polisi katika kaunti ndogo ya Rongo wanamsaka mwanamume mwenye umri wa miaka 37 anayedaiwa kumuua babake mzazi katika kijiji cha Nyangau kaunti ndogo ya Rongo, Kaunti ya Migori.
Ingawa haijafahamika ni kwa nini Geoffrey Agunga alimuua babake Agunga Riwa, wanafamilia wanakisia kuwa huenda inahusishwa na shilingi 200,000 ambazo mshukiwa alimpa dadake miezi kadhaa iliyopita.
Mwana wa marehemu Jason Ouma amesema kuwa Geoffrey amekuwa na ugomvi na wazazi wake kwa wiki kadhaa baada ya dadake kushindwa kumlipa pesa alizomkopesha alipokuwa bado anafanya kazi nchini Qatar.
Imetayarishwa na Janice Marete