GAVANA KIHIKA AWALAUMU WAKENYA KWA ‘KUWA NA MTAZAMO HASI, WABISHI NA WASIO WAZALENDO’

Gavana wa kaunti ya Nakuru Susan Kihika amewasuta Wakenya kwa kutopendezwa kwao na sera za utawala wa Rais William Ruto kuhusu kuinua hali ya uchumi wa nchi.
Katika chapisho refu kwenye jukwaa lake la kijamii, Kihika amehoji ni kwa nini umma umemkosoa rais william Ruto kwa kujaribu kutafuta pesa, ndani au nje ya nchi , kufadhili miradi mikubwa ya miundombinu.
Pia ameeleza kushangazwa na Wakenya kufuatia hatua yao ya kupinga mikataba ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPs); akitaja kuwa ni muhimu katika kushirikisha sekta binafsi kufadhili miradi ya mabilioni badala ya kutegemea hazina.
Imetayarishwa na Janice Marete