MANU MBIONI KUMNAYKUA AMORIM
Sporting Lisbon ilithibitisha nia ya Manchester United ya kutaka kumsajili kocha wao Mreno Ruben Amorim na nia yao ya kutimiza masharti yake ya kuachiliwa ya euro milioni 10.
United ilimtimua Erik ten Hag siku ya Jumatatu kufuatia mwanzo mbaya wa msimu, na kusababisha uvumi kuhusu mrithi wake.
Amorim mwenye umri wa miaka 39 alithibitishwa mara moja kuwa kipenzi chao ingawa meneja wa Brentford Thomas Frank na bosi wa Fulham Marco Silva pia waliripotiwa kuwa kwenye orodha hiyo.
Sporting, hata hivyo, ilitoa kiashiria kizito kwamba United walikuwa wanakaribia kulenga nambari moja.
Amorim alikataa kuzungumzia uvumi huo alipoulizwa Jumatatu usiku wa kuamkia mechi ya Kombe la Ligi ya Sporting dhidi ya Nacional.
Amorim, anayechukuliwa kuwa mmoja wa makocha bora zaidi barani Ulaya, alipendekezwa kuchukua nafasi ya Jurgen Klopp katika klabu ya Liverpool msimu huu, kabla ya Mholanzi Arne Slot hatimaye kuteuliwa.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































