#Local News

RUTO AELEKEA BURUNDI KWA MKUTANO WA COMESA

Rais William Ruto amesafiri hadi Burundi kuhudhuria Mkutano wa 23 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa COMESA mjini Bujumbura.

Katika taarifa ya msemaji wa ikulu Hussein Mohamed, mkutano wa mwaka huu utaadhimisha miaka 30 ya COMESA ambayo ni muungano muhimu wa kibiashara kwa bara hili.

Ikiwa na soko la pamoja la watu milioni 640 na Pato la Taifa la shilingi trilioni 128, COMESA inatoa soko kubwa kwa Kenya ambayo kwa sasa inashikilia asilimia 12.4 ya soko la kikanda, pili baada ya Misri.

Imetayarishwa na Janice Marete

RUTO AELEKEA BURUNDI KWA MKUTANO WA COMESA

KPSEA: FAMILIA ELDORET YASIKITIKIA MTIHANI

RUTO AELEKEA BURUNDI KWA MKUTANO WA COMESA

DUALE: MSWADA WA KUONGEZA MUHULA WA URAIS

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *