WAZAZI WATAKA HAKI KWA WANAO WALIOFANYA KPSEA GHUSHI

Wazazi ambao watoto wao walifanya mtihani ghushi wa KPSEA wanaitaka wizara ya eimu kuharakisha uchunguzi na vile vile kuwapa mwelekeo.
Wazazi wa Shule ya Silver Bells Academy huko Eldoret wamekashifu hatua ya wanao kufanyiwa mtihani ghushi wa Tathmini ya Elimu ya Shule ya Msingi ya Kenya (KPSEA).
Wakiongozwa na Wilson Ndege, wazazi hao sasa wanaitaka wizara ya elimu kuchunguza tukio hilo wakisema wamekuwa wakiwalipia watoto wao karo ya shule na sasa hatima yao haijulikani.
Kulingana na kamishna wa Kaunti Ndogo ya Moiben Duncan Okwach, imebainika kuwa taasisi hiyo ya kibinafsi iliyoko Kimumu Estate viungani mwa Eldoret haijasajiliwa na Wizara ya Elimu.
Okwach ameongeza kuwa watahiniwa 23 wa mitihani ya tathmini ya KPSEA katika shule hiyo hawakuwa wamesajiliwa pia.
Imetayarishwa na Janice Marete