#Football #Sports

MAN-U WATOA SARE YA 1-1DHIDI YA CHELSEA

Bao la Moises Caicedo la dakika ya 74 lilifuta bao la kwanza lake Brunoi Fernandez kunako dakika ya 70 kutoka eneo la Hatari. Bao hilo liliinyima Manchester United ushindi katika mechi yao ya kwanza ya Premier League tangu kumtimua kwa Erik ten Hag huku Chelsea ikiambulia sare ya 1-1.

Matokeo hayo yalimyima meneja wa united wa muda Ruud van Nistelrooy ushindi wake wa pili tangu kuchukua nafasi ya Erik Ten Hag kwa muda.

United imesalia katika nafasi ya 13 kwenye jedwali la ligi ya primia ikiwa na point 12 katika mechi 10 ikiwa ni mwanzo mbaya zaidi katika kampeni za ligi tangu mwaka wa 1986-1987.

Imetayarishwa na Janice Marete

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *