WASIMAMIZI WA KCSE WEBUYE WAONYWA
Katika juhudi za kuimarisha usalama na ubora wa mtihani wa kitaifa KCSE ambao umeanza hii leo, mkurugenzi wa elimu katika eneo bunge la Webuye Mashariki Dkt Paul Rono amewaonya wasimamizi wa mtihani huo dhidi ya ukiukaji wa mwongozo wa baraza la mitihani ya kitaifa KNEC ikiwemo kuwezesha udanganyifu.
Rono ametoa onyo hiyo akiwa mjini Webuye kabla ya zoezi la usambazaji wa mitihani hiyo mapema leo, alipokuwa ameandamana na naibu kamishna wa eneo hilo Peter Yegon.
Kulingana na Yegon, usalama umeimarishwa eneo hilo wakati na hata baada ya mtihani huo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































