#Local News

MAHAKAMA YA RUFAA KUSIKIZA KESI YA GACHAGUA DHIDI YA MAJAJI WA MAHAKAMA YA JUU

Mahakama ya Rufaa leo itasikiza kesi iliyowasilishwa na aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua akipinga kuhusika kwa benchi ya Mahakama Kuu inayosikiliza kesi yake dhidi ya kuondolewa kwake madarakani.

Gachagua alielekea katika Mahakama ya Rufaa akitaka amri ya kutangaza benchi ya majaji Eric Ogola, Anthony Mrima na Frida Mugambi kuwa kinyume na katiba akisema muundo wake ulifanywa na Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu wala si Jaji Mkuu Martha Koome inavyotakiwa.

Majaji wa Mahakama ya Rufaa Patrick Kiage, Aggrey Muchelule na George Odunga walikuwa wameagiza kesi hiyo isikizwe hii leo.

Kesi hiyo ilikuwa imepangwa kusikizwa Alhamisi wiki jana lakini ikaahirishwa hadi leo Jumatano, baada ya mahakama kufahamishwa kuwa mawakili wa Gachagua hawakuwa wamewasajili walalamikiwa wote na kuwapa stakabadhi.

Majaji hao waliagiza rufaa hiyo ifanyiwe marekebisho ili kuwanasa walalamikiwa wote kama ilivyoorodheshwa katika kesi iliyoko Mahakama Kuu na kwamba wote wahudumiwe.

Wahojiwa walielekezwa kuwasilisha majibu yao ifikapo Jumatatu kabla ya kusikilizwa kwa kesi hiyo leo.

Imetayarishwa na Janice Marete

MAHAKAMA YA RUFAA KUSIKIZA KESI YA GACHAGUA DHIDI YA MAJAJI WA MAHAKAMA YA JUU

LISBON WAWASHANGAZA MANCITY

MAHAKAMA YA RUFAA KUSIKIZA KESI YA GACHAGUA DHIDI YA MAJAJI WA MAHAKAMA YA JUU

MAAFISA WA ZAMANI NYS WAHUKUMIWA KIFUNGO GEREZANI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *