“MUNGU ALINIOKOA NIWAOKOE”- TRUMP

Rais mteule wa Marekani Donald Trump amesema kuwa Mungu aliokoa Maisha yake ili yeye aje kuokoa Marekani, akizungumza muda mfupi baada ya kuibuka mshindi kwenye uchaguzi mkuu nchini humo na kumpiku Kamala Harris wa chama cha Democrat.
Trump ambaye amekuwa mgombea wa chama cha Republican amepata ushindi mnono dhidi ya Harris aliyechukua nafasi ya Rais anayeondoka Joe Bidden, na kurejea katika Ikulu ya White House baada ya kupoteza kiti hicho kwenye uchaguzi wa mwaka 2020.
Ameahidi kutekeleza ahadi zake kwa wamarekani.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa