#Local News

‘MGENI’ WA GHAFLA DARASANI ASITISHA KCSE MOMBASA

Polisi katika kaunti ya Mombasa wanaendeleza uchunguzi katika kisa ambapo watahiniwa 5 wa mtihani wa KCSE katika shule ya wasichana Makande wamelazwa hospitalini baada yao kuvuta gesi iliyoenea darasani walipokuwa wakijitayarisha kwa mtihani huo.

Kwenye tukio hilo ambapo watahiniwa 8 wamezirai, walimu na maafisa wa polisi wamelazimika kusitisha mtihani kwa muda ili kuwaondoa wanafunzi shuleni humo.

Kwa mujibu wa mkurugenzi wa elimu eneo hilo Ali Aden, gesi hiyo imetoka nje ya shule, na polisi wanachunguza kubaini chanzo chake.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

‘MGENI’ WA GHAFLA DARASANI ASITISHA KCSE MOMBASA

29 BADO HAWAJULIKANI WALIKO, POLISI

‘MGENI’ WA GHAFLA DARASANI ASITISHA KCSE MOMBASA

WANAFUNZI WA GREDI YA TISA WAHAKIKISHIWA KUSOMA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *