WAZAZI WATAKIWA KUWAJIBIKIA MAISHA YA WANAO

Wazazi wametakiwa kuwa waangalifu na kuwajibikia malezi ya wanao wakati huu wa likizo ndefu.
Naibu kamishina wa webuye katika kaunti ya Bungoma Dickson Osundwa amewataka wazazi kuwaepusha wanao kuhudhuria hafla za disko matanga ambazo kulingana naye zimechangia ongezeko la uja ujito wa mapema kwqa wasichana.
Osundwa aidha amesikitikia ongezeko la dhuluma za kijinsia eneo hilo akiwashauri wanandoa kutafurta njia mwafaka za kusuluhisha migogoro baina yao katika juhudi za kupunguza visa vya dhuluma za kijinsia.
Imetayarishwa na Janice Marete