#Football #Sports

NETO AOKOA SARE YA CHELSEA HUKU JITIHADA ZA KUWANIA TAJI LA ARSENAL ZIKIPATA PIGO JIPYA

Pedro Neto aliipiga Arsenal pigo jipya katika mbio zao za ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza huku winga huyo wa Chelsea akifunga bao zuri na kuokoa sare ya 1-1 katika debi ya London jana Jumapili.

Timu ya Mikel Arteta ilikuwa imepata uongozi kupitia bao la Gabriel Martinelli katika kipindi cha pili kwenye uwanja wa Stamford Bridge.

Lakini bao la kusawazisha la Neto dakika 10 baadaye liliipatia Chelsea pointi iliyostahili na kuwaacha Arsenal bila ushindi katika mechi zao nne za ligi zilizopita. Bao hilo la Neto lilikuwa la kwanza katika Ligi Kuu tangu ahamie Chelsea kutoka Wolves mnamo Agosti, na liliweka Chelsea katika nafasi ya tatu juu ya Arsenal walioko nafasi ya nne kwa tofauti ya mabao.

Timu zote mbili ziko pointi tisa nyuma ya vinara Liverpool, lakini wakati Chelsea watatiwa moyo na nafasi yao baada ya kuvuka matarajio katika msimu wa kwanza wa Enzo Maresca kama kocha, Arsenal wanakwenda katika mapumziko ya kimataifa wakiwa na maswali kuhusu kupoteza mwelekeo.

Baada ya kufungwa 1-0 na Inter Milan kwenye Ligi ya Mabingwa Jumatano, siku chache tu baada ya kupoteza kwa Newcastle mwishoni mwa wiki iliyopita, Arsenal wamepata ushindi mara tatu tu katika mechi zao tisa za ligi zilizopita.

Imetayarishwa na Janice Marete

NETO AOKOA SARE YA CHELSEA HUKU JITIHADA ZA KUWANIA TAJI LA ARSENAL ZIKIPATA PIGO JIPYA

SHABANA YAILAZA KENYA POLICE FC BAO 1-0

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *