WADAU WAIBUA HOFU KUHUSU GREDI 9

Washikadau katika sekta ya elimu wameibua hofu kuhusiana na ukosefu wa utayari wa serikali kufanikisha masomo ya gredi ya 9 yanayoanza mwaka ujao, wakiitaka kuharakisha ujenzi wa madarasa na kuwaajiri walimu Zaidi wa sekondari msingi JSS.
Wadau hao wanaojumuisha walimu na wazazi kote nchini, wamesema hadi sasa hawajapokea orodha ya mahitaji ya mtaala wa gredi ya 9.
Hata hivyo, katibu katika wizara ya elimu Belio Kipsang amesema mikakati mwafaka imewekwa kufanikisha masomo hayo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa