BALOZI WHITMAN AJIUZULU

Balozi wa Marekani humu nchini Meg Whitman amejiuzulu, baada ya kuhudumu katika wadhifa huo tangu mwaka 2022.
Katika ujumbe wake, Whitman ambaye amekuwa akishinikizwa na vijana wa kizazi cha Gen Z kuondoka, amesema kuwa amewasilisha uamuzi wake kwa Rais wa Marekani anayeondoka Joe Bidden.
Uamuzi wake wa kujiuzulu umejiri takribani wiki moja baada ya ushindi wa Donald Trump kwenye uchaguzi wa urais.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa