WANASIASA CHIPUKIZI WATETEA BEI YA SHILINGI 3500 INAYONUIWA KUNUNUA MAHIDI YA GUNIA YA KILO TISISNI NA SERIKALI

Wanasiasa chipukizi katika kaunti ya Transnzoia wametamaushwa na hatua ya serikali kupunguza bei ya mahidi gunia moja ya kilo 90 kutoka 4000 hadi 3500.
Kulingana na wanasiasa hao wakulima waliuziwa mbolea ya bei nafuu isiyoafikia ubora wa viwango vinavyohitajika na wizara ya kukadiria ubora wa bidhaa KEBS huku wakitoa wito kwa rais William Ruto kuingilia kati ili wakulima wasipate hasara kutokana na gharama ya juu ya uzalishaji.
Wanasiasa hao aidha wameitaka serikali kutafakari nia yao ya kununuja magunia milioni 1 ya mahidi kwa kuwa kulingana nao wakulima wanatarajiaa kuzalisha mahindi mengi mwaka huu.
Imetayarishwa na Janice Marete