MGOMO VYUONI: OMTATAH ASHINIKIZA MAZUNGUMZO

Wakati uo huo, wito unaendelea kutolewa kwa serikali kutafuta suluhu kwa mgomo wa wahadhiri na kuwaepushia wanafunzi wa vyuo vikuu vya masaibu yanayowakumba ikiwemo kukaa vyuoni kwa muda mrefu Zaidi ya kawaida kabla ya kuhitimisha masomo yao.
Wa hivi ni seneta wa Busia Okiya Omtatah ambaye ameutaja mgomo wa wahadhiri unaoendelea kama ambao umefikia hatua mbaya, na kuhimiza mazungumzo baina ya serikali na wahadhiri.
Kupitia mtandao wa kijamii wa X, Omtatah amesikitikia mahangaiko ya wanafunzi na kuwataka wahusika kuwaangazia.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa