#Football #Sports

NAIROBI UNITED YASHINDA APS 1-0

Nairobi United ilishinda 1-0 dhidi ya Administration Police Service (APS) Bomet na kusimamisha mbio zao nzuri katika Ligi Kuu ya Taifa.

Nairobi United ilifunga kupitia kijana Dancun Omalla, ambaye aliongeza idadi yake ya mabao kuwa matano, baada ya michezo tisa.

Kocha wa Nairobi United, Edwin Mwaura, amesema bado hawajafika wanapotaka kuwa licha ya ushindi mdogo.

Mwaura amemsifia Omalla kwa kwa kipaji cha kipekee huku najiandaa kwa mambo makubwa zaidi katika siku zijazo.Baada ya ushindi huo, Nairobi United ilifikia pointi 19 kwenye jedwali.

Fortune Sacco ilidumisha uongozi wao kileleni baada ya ushindi mgumu wa 1-0 dhidi ya SS Assad.

Derbi ya Mombasa kati ya Mombasa Stars na Mombasa United ilimalizika kwa sare ya bila kufungana kwenye uwanja wa Serani.

Kisumu All Stars walipigana vikali na kumaliza kwa sare ya 0-0 dhidi ya Muhoroni Youth, huku Naivas na Kibera Black Stars pia wakimaliza kwa sare ya 0-0.

Imetayarishwa na Janice Marete

NAIROBI UNITED YASHINDA APS 1-0

MWAURA ATETEA SERIKALI DHIDI YA KUFELI, MSWADA

NAIROBI UNITED YASHINDA APS 1-0

SIMBAS WAANGAZIA KOMBE LA AFRIKA 2025 BAADA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *