FEDHA ZA KAUNTI: SIFUNA APENDEKEZA BUNGE KUVUNJWA

Utata kuhusu madai ya kucheleweshwa kwa fedha za kaunti umechukua mkondo tofauti, seneta wa Nairobi Edwin Sifuna akipendekeza kuvunjwa kwa bunge la kitaifa iwapo maamuzi muhimu ya bunge hilo yatakuwa yakifanywa na serikali tendaji.
Amekuwa akirejelea kauli za waziri wa fedha John Mbadi kwamba serikali za kaunti hazitaongezewa mgao wa fedha jinsi maseneta walivyopendekeza.
Haya yanajiri wakati ambapo seneti inatarajiwa kujadili mswada wa ugavi wa mapato ili kuondoa mtafaaruku kuhusu mgao wa kaunti.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa