MRADI WA UMEME WAZINDULIWA BUNGOMA

Shughuli za masomo, viwanda na usalama katika kaunti ya Bungoma zimepigwa jeki baada ya kaunti hiyo kuzindua mradi wa usambazaji umeme katika kaunti zote 45, utakaogharimu shilingi milioni 90.
Mradi huo unaendeshwa na serikali ya kaunti ya Bungoma kwa ushirikiano na shirika la REREC, gavana Ken Lusaka akielelezea matumaini ya kuboreshwa kwa Maisha ya wakazi kupitia mradi huo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi kwenye eneo bunge la Kanduyi, Lusaka amewataka wakazi kutunza miundo msingi ya mradi huo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa