AFUENI YA NG-CDF KHWISERO

Ni afueni kwa wakazi wa eneo bunge la Khwisero kaunti ya Kakamega baada ya hazina ya ustawishaji wa eneo bunge hilo NG-CDF kutenga kima cha shilingi milioni 35 kugharamia karo ya wanafunzi wa shule za kutwa.
Mbunge wa eneo hilo Christopher Aseka amesema kuwa tayari shilingi milioni 8 zimetengwa kufanikisha mpango huo kwa awamu ya kwanza, wazazi wakihitajika kulipa shilingi 1,000 kama karo ya muhula.
Kulingana naye, mpango huo unalenga kuimarisha usawa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa