#Local News

KINDIKI: SERIKALI KUZINDUA MAENEO YA BIASHARA KILA KAUNTI

Huenda shughuli za kibiashara na kilimo zikaimarika kote nchini iwapo serikali kuu itatimiza ahadi yake ya kuzindua kati ya maeneo 6-10 ya biashara na uzalishaji katika kaunti zote 47 kufikia mwisho wa mwaka huu.

Akizungumza katika kikao na magavana 19 kutoka kaunti 19 ambazo zimeorodheshwa kwa ujenzi wa maeneo maalum`ya biashara katika awamu ya kwanza ya mpango huo, naibu rais Kithure Kindiki amesema fedha zilizotengwa ni sharti zitumike ipasavyo.

Aidha, amewarai magavana kuwajibika na kutoa mgao wao katika ujenzi wa maeneo hayo.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

KINDIKI: SERIKALI KUZINDUA MAENEO YA BIASHARA KILA KAUNTI

EACC YAPATA MKUU MPYA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *