#Local News

MHUDUMU WA MPESA APIGWA RISASI KATIKA TUKIO LA UHALIFU MUKURWEINI NYERI

Polisi wanaendelea kuwasaka watu waliompiga risasi Mhudumu wa Mpesa na kujeruhiwa katika tukio la wizi katika Mji wa Kiahungu, Kaunti ya Nyeri.

Kulingana na polisi, mwanamke huyo alikuwa akirejea nyumbani baada ya shughuli za siku, akiwa na mwenzake, walipovamiwa na wanaume wawili, mmoja akiwa na bastola.

Wahalifu walimnyang’anya KSh.160,000 taslimu, simu tatu, na bidhaa mbalimbali kabla ya kumpiga risasi mguuni alipojaribu kupinga wizi huo. Walitoroka wakimwacha mwathiriwa akivuja damu, huku mwanamke aliyekuwa naye akitoroka bila kujeruhiwa.

Mwathiriwa amekimbizwa katika Hospitali ya Mukurweini Sub-County kwa matibabu na hali yake imeripotiwa kuwa imara. Polisi wanasema juhudi za kuwasaka wahusika zinaendelea.

Imetayarishwa na Janice Marete

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *