MWANAMKE AZUILIWA JUJA KWA KUMCHOMA KISU MPENZI WAKE

Polisi huko Juja wanamzuilia Cynthia Nakato, mwenye umri wa miaka 20, kwa madai ya kumchoma kisu mara saba mpenzi wake Peter Macharia, 23, na kusababisha kifo chake katika eneo la Mastore, Juja, Januari 20, 2024.
Mwili wa marehemu umepelekwa katika chumba cha maiti kwa uchunguzi wa baada ya kifo, huku polisi wakisema uchunguzi unaendelea.
Kamanda wa Polisi wa Juja, Jackson Sang, amewataka wanandoa vijana kutafuta njia za amani kutatua migogoro yao.
Imetayarishwa na Janice Marete