#Sports #Volleyball

KENYA PRISONS YASHINDA KAPU KATIKA MTANANGE MKALI WA KVF

Kenya Prisons walilazimika kupambana kwa nguvu ili kushinda Kenya Airport Police Unit (KAPU) kwa seti 3-2 kwenye Ligi ya Taifa ya Wanaume ya Shirikisho la Voliboli Kenya (KVF), wakirejea kwenye njia ya ushindi baada ya kupoteza dhidi ya GSU siku ya Jumamosi katika Ukumbi wa Nyayo.

Prisons walipoteza kwa seti 3-2 dhidi ya mabingwa wa zamani GSU, ikiwa ni kichapo chao cha kwanza msimu huu, lakini walijikakamua na kushinda KAPU, wakipata alama mbili na kuongoza msimamo wa ligi kwa alama 26.

Kikosi cha kocha Dennis Mokua kilianza kwa kishindo kwa kushinda seti ya kwanza 25-14, lakini KAPU walijibu mapigo kwa kushinda seti ya pili 25-20. Hata hivyo, Prisons walirejea mchezoni na kushinda seti ya tatu 25-22.

KAPU walionyesha ushindani mkali kwa kusawazisha tena kwa kushinda seti ya nne 25-21, na kulazimisha seti ya mwisho kuamua mshindi. Katika seti ya mwisho, Prisons walidhibiti presha na kushinda 15-13 katika mechi iliyowasisimua mashabiki.

Akizungumza baada ya mechi, nahodha wa Prisons, Jairus Kipkosgey, alikiri ugumu wa mchezo huo na umuhimu wa mafunzo waliyopata.

Imetayarishwa na Janice Marete

KENYA PRISONS YASHINDA KAPU KATIKA MTANANGE MKALI WA KVF

TUSKER FC YASIMAMA KIDETE DHIDI YA USM

KENYA PRISONS YASHINDA KAPU KATIKA MTANANGE MKALI WA KVF

GUARDIOLA AKEMEA UDHAIFU WA MAN CITY BAADA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *