#Football #Sports

TUSKER FC YASIMAMA KIDETE DHIDI YA USM ALGER KWA RYAN OGAM

Ryan Ogam wa Tusker FC bado analengwa na USM Alger ya Algeria kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili siku ya Jumatano, lakini klabu yake imeapa kutomwachia.

Ogam, aliye na mwaka mmoja na nusu kwenye mkataba wake, ameivutia Alger baada ya kufunga mabao 15 katika mechi 14. Hata hivyo, Tusker wanapinga uhamisho wake kwa madai kwamba Alger ilimfuata moja kwa moja kabla ya kuwasiliana na klabu.

Tusker wanatishia kuchukua hatua za kisheria iwapo Alger wataendelea na mpango huo. Licha ya sintofahamu, Ogam ameendelea na mazoezi na yupo kwenye kikosi kitakachomenyana na KCB FC

Kocha Charles Okere ana imani kuwa mshambuliaji huyo ataendelea kuonyesha makali yake na kusaidia timu kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya FKF.

Imetayarishwa na Janice Marete

TUSKER FC YASIMAMA KIDETE DHIDI YA USM ALGER KWA RYAN OGAM

WABUNGE WALALAMIKIA HUDUMA DUNI ZA SHA

TUSKER FC YASIMAMA KIDETE DHIDI YA USM ALGER KWA RYAN OGAM

KENYA PRISONS YASHINDA KAPU KATIKA MTANANGE MKALI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *