IDARA YA UHAMIAJI YAWATAKA WAKENYA WACHUKUE VITAMBULISHO

Wakenya waliotuma maombi ya kupata vitambulisho vya kitaifa wameshauriwa kuzuru vituo vya uhamiaji nchini na kuchukua stakabadhi hizo, serikali ikisema takribani ya vitambulisho elfu 500 vingali katika vituo hivyo.
Kwa mujibu wa katibu katika idara ya uhamiaji Julius Bitok, Zaidi ya kadi milioni 3 za Maisha zimekabidhiwa waliotuma maombi kufikia sasa, na kuwataka wakenya kujitokeza ili kuchukua stakabadhi hizo muhimu.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa