MGOMO: WAGONJWA MTRH WAHANGAIKA

Shughuli za matibabu katika hospitali ya rufaa na mafunzo ya Moi jijini Eldoret zimesambaratika kutokana na mgomo wa madaktari ambao umeanza hii leo, madaktari wakiapa kutorejea kazini hadi malalamishi yao yatakapoangaziwa.
Miongoni mwa malalamishi ya madaktari hao ni wenzao kukaa kwa mkataba kwa muda mrefu bila kupewa ajira ya kudumu.
Haya yanajiri huku wagonjwa wakihangaika kutokana na kukwama kwa shughuli zote za matibabu.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa