SERIKALI YAOMBWA KUKABILI FUNZA KAKAMEGA

Serikali ya kaunti ya Kakamega na ile ya kitaifa zimetakiwa kuingilia kati na kusaidia katika kupambana na janga la funza kwenye shule za kaunti hiyo, ambalo linahofiwa kushusha viwango vya masomo.
Wakizungumza baada ya juhudi za kuangamiza funza miongoni mwa wanafunzi katika maeneo ya Butere, Navakholo, Khwisero na Mumias Magharibi viongozi wakiwemo walimu wakuu wa shule za maeneo hayo wamesema wadudu hao wamekuwa tishio kwa vipindi vya masomo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa