MTEGO WA STIMA PLAZA: WAWILI WAFUTWA KAZI

Maafisa wawili wakuu katika serikali ya kaunti ya Nairobi wamesimamishwa kazi wakidaiwa kutoa maagizo kwa madereva wa malori ya kuzoa taka kutupa taka nje ya jengo la Stima Plaza wakati wa mzozo baina ya serikali hiyo na kampuni ya Kenya Power.
Haya ni kwa mujibu wa gavana Johnson Sakaja, ambaye amezungumza akiwa mbele ya kamati ya usalama na utawala katika bunge la kitaifa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa